John 1:19-24

19 aHuu ndio ushuhuda wa Yahya wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20 bYahya alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Al-Masihi.”
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.

21 dWakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Ilya?”

Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.”

“Je, wewe ni yule Nabii?”

Akajibu, “Hapana.”

22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”

23 eAkawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ”

24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo
Copyright information for SwhKC