John 13:21-26

21 aBaada ya kusema haya, Isa alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”

22Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. 23 bMmoja wa wanafunzi wake ambaye Isa alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Isa. 24Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.”

25 cYule mwanafunzi akamwegemea Isa, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?”

26 dIsa akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.” Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni.
Copyright information for SwhKC