John 18:2-7

2 aBasi Yuda, yule aliyemsaliti alipafahamu mahali hapo kwani Isa alikuwa akikutana humo na wanafunzi wake mara kwa mara. 3 bHivyo Yuda akaja bustanini. Aliongoza kikosi cha askari wa Kirumi, na baadhi ya maafisa kutoka kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo. Nao walikuwa wamechukua taa, mienge na silaha.

4 cIsa akijua yale yote yatakayompata, akajitokeza mbele yao akawauliza, “Mnamtafuta nani?”

5 dWao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.”

Isa akawajibu, “Mimi ndiye.” Yuda, yule aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
6Isa alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi nyuma na kuanguka chini!

7 eAkawauliza tena, “Mnamtafuta nani?”

Nao wakamjibu, “Isa Al-Nasiri.”

Copyright information for SwhKC