Joshua 1:1-6

Bwana Anamwagiza Yoshua

1 aBaada ya kifo cha Musa mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa: 2 b“Mtumishi wangu Musa amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli. 3 cKila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Musa. 4 dNchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa
Yaani Bahari ya Mediterania.
iliyoko upande wa magharibi.
5 fHakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.

6 g“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa.
Copyright information for SwhKC