Joshua 18:1-6

Mgawanyo Wa Nchi Iliyobaki

1 aKusanyiko lote la Waisraeli likakusanyika huko Shilo na kusimamisha Hema la Kukutania. Nchi ikawa chini ya utawala wao, 2lakini palikuwa bado makabila saba ya Israeli ambayo yalikuwa hayajapokea urithi wao.

3 bHivyo Yoshua akawaambia Waisraeli, “Je, mtasubiri hata lini ili kuingia kumiliki nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? 4 cChagueni watu watatu kutoka kwenye kila kabila. Nitawatuma hao watu kukagua hiyo nchi na kuniandikia mapendekezo ya mgawanyo wa urithi wa kila kabila. Nao watanirudia. 5 dMtaigawanya hiyo nchi katika sehemu saba. Yuda atabaki katika eneo lake upande wa kusini na nyumba ya Yusufu katika nchi yake upande wa kaskazini. 6 eBaada ya kuandika maelezo ya hizo sehemu saba za nchi, yaleteni kwangu, nami nitawapigia kura kwa kura mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wetu.
Copyright information for SwhKC