Leviticus 11:1-6

Vyakula Najisi Na Visivyo Najisi

(Kumbukumbu 14:3-21)

1 Bwana akawaambia Musa na Haruni, 2 a“Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala: 3Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

4“ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu. 5Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. 6 bSungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.
Copyright information for SwhKC