Luke 1:46-51

46 aNaye Mariamu akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47 bnayo roho yangu inamfurahia
Mungu Mwokozi wangu,

48 ckwa kuwa ameangalia kwa fadhili
unyonge wa mtumishi wake.
Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,

49 dkwa maana yeye Mwenye Nguvu
amenitendea mambo ya ajabu:
jina lake ni takatifu.

50 eRehema zake huwaendea wale wamchao,
kutoka kizazi hadi kizazi.

51 fKwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake;
amewatawanya wale wenye kiburi
ndani ya mioyo yao.
Copyright information for SwhKC