Luke 11:14-19

14 a bBasi Isa alikuwa anamtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu aliyekuwa bubu. Yule pepo mchafu alipomtoka yule mtu aliyekuwa bubu, akaanza kuongea, nao umati wa watu ukashangaa. 15 cLakini wengine wakasema, “Anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli,
Beelzebubu au Beelzebuli; ni mkuu wa pepo wachafu; pia 18, 19.
yule mkuu wa pepo wachafu wote.”
16 eWengine ili kumjaribu wakataka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17 fIsa akajua mawazo yao, naye akawaambia, “Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Nayo nyumba iliyogawanyika dhidi yake yenyewe itaanguka. 18 gKama Shetani amegawanyika mwenyewe, ufalme wake utasimamaje? Nawaambia haya kwa sababu ninyi mnadai ya kuwa mimi ninatoa pepo wachafu kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 hKama mimi natoa pepo wachafu kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu nao je, wao hutoa pepo wachafu kwa uwezo wa nani? Hivyo basi, wao ndio watakaowahukumu.
Copyright information for SwhKC