Luke 14:15-20

15 aMmoja wa wale waliokuwa pamoja naye mezani aliposikia hivi akamwambia Isa, “Amebarikiwa mtu yule atakayekula katika karamu ya Ufalme wa Mungu!”

16 bIsa akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 17 cWakati wa karamu ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaambie wale walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ki tayari sasa.’

18“Lakini wote, kila mmoja, wakaanza kutoa udhuru: Wa kwanza akasema, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’

19“Mwingine akasema, ‘Ndipo tu nimenunua jozi tano za ng’ombe wa kulimia, nami ninakwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 20 dNaye mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

Copyright information for SwhKC