Luke 14:25-30

25Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukisafiri pamoja na Isa, naye akageuka, akawaambia, 26 a“Mtu yeyote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto wake, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe. 27 bYeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

28 c“Ni nani miongoni mwenu ambaye kama anataka kujenga nyumba, hakai kwanza chini na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha? 29La sivyo, akiisha kuweka msingi, naye akiwa hana uwezo wa kuikamilisha, wote waionao wataanza kumdhihaki, 30wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini hakuweza kukamilisha.’

Copyright information for SwhKC