Luke 22:39-44

39 aIsa akatoka, akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata. 40 bWalipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” 41 cAkajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42 dakisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 43 eMalaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 fNaye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

Copyright information for SwhKC