Luke 23:18-23

18 aNdipo watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “Mwondoe mtu huyo! Tufungulie Baraba!” 19(Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya maasi yaliyokuwa yametokea mjini, na kwa ajili ya uuaji).

20Pilato, akitaka kumwachia Isa, akasema nao tena. 21Lakini wao wakaendelea kupiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!”

22 bKwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”

23Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu zaidi, wakidai kwamba Isa asulubiwe. Hivyo, kelele zao zikashinda.
Copyright information for SwhKC