Luke 5:27-32

27 aBaada ya haya, Isa alitoka na kumwona mtoza ushuru mmoja jina lake Lawi akiwa amekaa forodhani, mahali pake pa kutoza ushuru. Akamwambia, “Nifuate.” 28 bNaye Lawi akaacha kila kitu, akaondoka, akamfuata.

29 cKisha Lawi akamfanyia Isa karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao. 30 dLakini Mafarisayo na walimu wa sheria waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Isa, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

31Isa akawajibu, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. 32 eSikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.”

Isa Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22)

Copyright information for SwhKC