‏ Luke 6:20-23

20 aAkawatazama wanafunzi wake, akasema: “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini,
kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

21 bMmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa,
kwa sababu mtashibishwa.
Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa,
kwa sababu mtacheka.

22 cMmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia,
watakapowatenga na kuwatukana
na kulikataa jina lenu kama neno ovu,
kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

23 d“Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.
Copyright information for SwhKC