Luke 6:6-11

6 aIkawa siku nyingine ya Sabato, Isa aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. 7 bMafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. 8 cLakini Isa alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.

9Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?”

10 dAkawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukaponywa kabisa. 11 eWale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Isa.

Isa Achagua Mitume Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:1-4; Marko 3:13-19)

Copyright information for SwhKC