Luke 9:18-21

18 aWakati mmoja, Isa alipokuwa akiomba faraghani, nao wanafunzi wake wakiwa pamoja naye, akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

19 bWakamjibu, “Baadhi husema wewe ni Yahya Mbatizaji, wengine husema ni Ilya, na bado wengine husema kwamba ni mmoja wa manabii wa kale amefufuka kutoka kwa wafu.”

20 cKisha akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”

Petro akajibu, “Wewe ndiwe Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
wa Mungu.”

21 eIsa akawakataza wasimwambie mtu yeyote jambo hilo.
Copyright information for SwhKC