Luke 9:7-9

7 aBasi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yahya Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu. 8 bWengine wakasema Ilya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. 9 cHerode akasema, “Yahya nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ambaye ninasikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona.

Isa Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Marko 6:30-44; Yohana 6:1-14)

Copyright information for SwhKC