Mark 11:1-6

Isa Aingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Mathayo 21:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

1 aWalipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage na Bethania katika Mlima wa Mizeituni. Isa akawatuma wawili wa wanafunzi wake, 2 bakawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na hapo mtakapoingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. 3 cKama mtu yeyote akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji, na atamrudisha hapa baada ya muda mfupi.’ ”

4 dWakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa kando ya barabara, karibu na mlango wa nyumba. 5Walipokuwa wanamfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakawauliza, “Mna maana gani mnapomfungua huyo mwana-punda?” 6Wakawajibu kama vile Isa alivyokuwa amewaagiza, nao wale watu wakawaruhusu.
Copyright information for SwhKC