Mark 14:22-26

22 aWalipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

23 bKisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

24 cAkawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25 dAmin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

26 eWalipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

Isa Atabiri Kuwa Petro Atamkana

(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

Copyright information for SwhKC