Mark 14:27-31

27 aIsa akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo watatawanyika.’

28 bLakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

29 cPetro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

30 dIsa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

31 eLakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Isa Aomba Katika Bustani Ya Gethsemane

(Mathayo 26:36-46; Luka 22:39-46)

Copyright information for SwhKC