Mark 15:1-5
Isa Mbele Ya Pilato
(Mathayo 27:1-14; Luka 23:1-5; Yohana 18:28-38)
1 aAsubuhi na mapema, viongozi wa makuhani, pamoja na wazee, walimu wa sheria na Baraza lote, wakafikia uamuzi. Wakamfunga Isa, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 bPilato akamuuliza, “Je, wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Isa akajibu, “Wewe umesema.” 3Viongozi wa makuhani wakamshtaki kwa mambo mengi. 4 cPilato akamuuliza tena, “Je, huna la kujibu? Tazama ni mashtaka mangapi wanayaleta juu yako.” 5 dLakini Isa hakujibu lolote, hivyo Pilato akashangaa.Pilato Amtoa Isa Asulubiwe
(Mathayo 27:15-26; Luka 23:13-25; Yohana 18:39–19:16)
Copyright information for
SwhKC