Mark 15:21-26

21 aMtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, baba yao Iskanda na Rufo, alikuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shamba, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 22 bKisha wakampeleka Isa mpaka mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 23 cNao wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini hakuinywa. 24 dBasi wakamsulubisha, nazo nguo zake wakagawana miongoni mwao kwa kuzipigia kura ili kuamua ni gani kila mtu ataichukua.

25 eIlikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 fTangazo likaandikwa la mashtaka dhidi yake lenye maneno haya: “Mfalme wa Wayahudi.”
Copyright information for SwhKC