Mark 3:1-6

Mtu Aliyepooza Mkono Aponywa

(Mathayo 12:9-14; Luka 6:6-11)

1 aIsa akaingia tena ndani ya sinagogi, na huko palikuwa na mtu aliyepooza mkono. 2 bWakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. 3Isa akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”

4Kisha Isa akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza kimya.

5 cIsa akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa! 6 dKisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya shauri la kumuua Isa wakiwa na Maherode.

Umati Wa Watu Wamfuata Isa

Copyright information for SwhKC