Matthew 1:1-6
Kumbukumbu Za Ukoo Wa Isa Al-Masihi
(Luka 3:23-38)
1 aHabari za ukoo wa Isa Al-Masihi mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu:2 bIbrahimu akamzaa Isaka,
Isaka akamzaa Yakobo,
Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,
3 cYuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
Peresi akamzaa Hesroni,
Hesroni akamzaa Aramu,
4 Aramu akamzaa Aminadabu,
Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni,
5 dSalmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,
Obedi akamzaa Yese,
6 eYese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.
Daudi akamzaa Sulemani, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.
Copyright information for
SwhKC