Matthew 10:5-10

5 aHawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria. 6 bLakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 7 cWakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ 8 dPonyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. 9 eMsichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu. 10 fMsichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.

Copyright information for SwhKC