Matthew 14:13-18

13 aIsa aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 14 bIsa alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

15 cIlipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

16Isa akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”

17 dWakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.”
Copyright information for SwhKC