Matthew 24:1-6

Kubomolewa Kwa Hekalu Kwatabiriwa

(Marko 13:1-2; Luka 21:5-6)

1 aIsa akatoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya Hekalu. 2 bNdipo Isa akawauliza, “Je, mnayaona haya yote? Amin, nawaambia, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”

Ishara Za Nyakati Za Mwisho

(Marko 13:3-23; Luka 21:7-24)

3 cIsa alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?”

4 dIsa akawajibu, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5 eKwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Al-Masihi,’
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
nao watawadanganya wengi.
6 gMtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado.
Copyright information for SwhKC