Matthew 27:32-37

32 aWalipokuwa wakienda, wakakutana na mtu mmoja kutoka Kirene, jina lake Simoni, nao wakamlazimisha kuubeba ule msalaba. 33 bWakafika mahali palipoitwa Golgotha (maana yake ni Mahali pa Fuvu la Kichwa). 34 cHapo wakampa Isa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini alipoionja, akakataa kuinywa. 35 dWalipokwisha kumsulubisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. [Hili lilifanyika ili litimie lile neno lililonenwa na nabii, “Waligawa nguo zangu miongoni mwao na vazi langu wakalipigia kura.”] 36 eKisha wakaketi, wakamchunga. 37 fJuu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake hivi: Huyu ni Isa, Mfalme wa Wayahudi.
Copyright information for SwhKC