Matthew 3:1-5

Yahya Mbatizaji Atayarisha Njia

(Marko 1:1-8; Luka 3:1-18; Yohana 1:19-28)

1 aSiku hizo Yahya Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Uyahudi, akisema, 2 b“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.” 3 cHuyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema: “Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ”

4 dBasi Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 eWatu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani.
Copyright information for SwhKC