Matthew 9:1-3
Isa Amponya Mtu Aliyepooza
(Marko 2:1-12; Luka 5:17-26)
1 aIsa akaingia kwenye chombo, akavuka na kufika katika mji wa kwao. 2 bWakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa.” 3 cKwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa sheria wakasema mioyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!”
Copyright information for
SwhKC