‏ Nehemiah 5:13

13 aPia nikakung’uta makunjo ya vazi langu na kusema, “Kila mtu ambaye hatatimiza ahadi hii, Mungu na amkung’ute hivi kutoka nyumba yake na katika mali zake. Basi mtu wa namna hiyo akung’utiwe nje na aachwe bila kitu!”

Waliposikia hili, mkutano wote ukasema, “Amen,” na wakamtukuza Bwana. Nao watu wakafanya kama walivyokuwa wameahidi.

Copyright information for SwhKC