Numbers 14:29-34

29 aKila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenung’unika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. 30 bHakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. 31 cLakini watoto wenu ambao mlisema watachukuliwa kama mateka, nitawaingiza humo ili waifurahie nchi ambayo ninyi mmeikataa. 32 dLakini ninyi, miili yenu itaanguka katika jangwa hili. 33 eWatoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili. 34 fKwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’
Copyright information for SwhKC