Numbers 14:40-44

40 aMapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahali Bwana alipotuahidi.”

41 bLakini Musa akasema, “Kwa nini hamtii amri ya Bwana? Jambo hili halitafanikiwa! 42 cMsipande juu, kwa kuwa Bwana hayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu, 43 dkwa kuwa Waamaleki na Wakanaani watapambana nanyi huko. Kwa sababu mmemwacha Bwana, hatakuwa pamoja nanyi, ninyi mtaanguka kwa upanga.”

44 eHata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Musa hakutoka kambini wala Sanduku la Agano la Bwana.
Copyright information for SwhKC