Numbers 16:17-22

17 aKila mtu atachukua chetezo chake na kuweka uvumba ndani yake, vyetezo 250 kwa jumla, na kukileta mbele za Bwana. Wewe na Haruni mtaleta vyetezo vyenu pia.” 18Kwa hiyo kila mtu akachukua chetezo chake, akaweka moto na uvumba ndani yake, na kusimama pamoja na Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania. 19 bKora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Musa na Haruni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu wa Bwana ukatokea kwa kusanyiko lote. 20Bwana akamwambia Musa na Haruni, 21 c“Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

22 dLakini Musa na Haruni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”

Copyright information for SwhKC