‏ Numbers 27:1-6

Binti Wa Selofehadi

1 aBinti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yusufu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia 2 bingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Musa, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko lote, wakasema, 3 c“Baba yetu alikufa jangwani. Hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora, ambao walifungamana pamoja dhidi ya Bwana, lakini alikufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe na hakuacha wana. 4Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”

5 dKwa hiyo Musa akalileta shauri lao mbele za Bwana, 6naye Bwana akamwambia Musa,
Copyright information for SwhKC