Numbers 28:1-6
Sadaka Za Kila Siku
(Kutoka 29:38-46)
1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’ 3 bWaambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku. 4 cAndaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni, 5 dkila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ▼▼ Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja.
ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ▼▼ Robo ya hini ni sawa na lita moja.
ya mafuta ya zeituni. 6 gHii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
Copyright information for
SwhKC