Numbers 28:16-21

16 a“ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana. 17 bKatika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. 18 cKatika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida. 19 dLeteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 20 ePamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa; 21pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.
Copyright information for SwhKC