‏ Numbers 5:1-4

Utakaso Wa Kambi

1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, ▼
▼ Ugonjwa wa ngozi uambukizao hapa ina maana ya ukoma.
au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.
3 cHii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.” 4Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile Bwana alivyokuwa amemwelekeza Musa.

Malipo Kwa Ajili Ya Makosa

Copyright information for SwhKC