Numbers 9:1-6

Pasaka Huko Sinai

1 a Bwana akasema na Musa katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema, 2 b“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. 3 cAdhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

4 dHivyo Musa akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka, 5 enao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Bwana alivyomwamuru Musa.

6 fLakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Musa na Haruni siku ile ile,
Copyright information for SwhKC