Proverbs 14:1-6
1 aMwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
2 bYeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.
3 cMazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake.
4 dPale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.
5 eShahidi mwaminifu hadanganyi,
bali shahidi wa uongo humimina uongo.
6 fMwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.
Copyright information for
SwhKC