‏ Proverbs 4:5-8


5 aPata hekima, pata ufahamu;
usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.

6 bUsimwache hekima naye atakuweka salama;
mpende, naye atakulinda.

7 cHekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.
Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.

8 dMstahi, naye atakukweza;
mkumbatie, naye atakuheshimu.
Copyright information for SwhKC