Proverbs 5:1-6

Onyo Dhidi Ya Uzinzi


1 aMwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu,
sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,

2 bili uweze kutunza busara
na midomo yako ihifadhi maarifa.

3 cKwa maana midomo ya mwanamke kahaba
hudondoza asali,
na maneno ya kinywa chake
ni laini kuliko mafuta;

4 dlakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,
mkali kama upanga ukatao kuwili.

5 eMiguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;
hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.
Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.


6 gYeye hafikiri juu ya njia ya uzima;
njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

Copyright information for SwhKC