Psalms 112:2-7


2 aWatoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

3 bNyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.

4 cHata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.


5 dMema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.

6 eHakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

7 fHataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
Copyright information for SwhKC