Psalms 135:15-18


15 aSanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

16 bZina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;

17 czina masikio, lakini haziwezi kusikia,
wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.

18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

Copyright information for SwhKC