Psalms 6:1-6

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu

(Kwa Mwimbishaji: Kwa Ala Za Nyuzi Za Muziki. Mtindo Wa Sheminithi.
Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji.
Zaburi Ya Daudi)


1 bEe Bwana, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

2 cUnirehemu Bwana,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Bwana, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.

3 dNafsi yangu ina uchungu mwingi.
Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?


4 eGeuka Ee Bwana, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

5 fHakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa kuzimu?


6 gNimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha nafurikisha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha viti vyangu vya fahari
kwa machozi.
Copyright information for SwhKC