Romans 11:1-6

Mabaki Ya Israeli

1 aBasi nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Ibrahimu kutoka kabila la Benyamini. 2 bMungu hajawakataa watu wake, ambao yeye aliwajua tangu mwanzo. Je, hamjui yale Maandiko yasemayo kuhusu Ilya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Israeli? 3 cAlisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?” 4 dJe, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.” 5 eVivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu. 6 fLakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.

Copyright information for SwhKC