Romans 14:13-18

13 aKwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine. 14 bNinajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Isa kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15 cKama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Al-Masihi alikufa kwa ajili yake. 16 dUsiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17 eKwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18 fKwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Al-Masihi kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.

Copyright information for SwhKC