Romans 6:2-7
2 aLa hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? 3 bAu hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Al-Masihi Isa tulibatizwa katika mauti yake? 4 cKwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Al-Masihi alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima. 5 dKwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. 6 eKwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. 7 fKwa maana mtu yeyote aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
Copyright information for
SwhKC