‏ 1 Chronicles 1

Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu

(Mwanzo 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)

Adamu Hadi Wana Wa Noa

1Adamu, Sethi, Enoshi, 2Kenani, Mahalaleli, Yaredi, 3Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

4Wana wa Noa walikuwa:
Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi

5Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
6Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
7Wana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

Wana Wa Hamu

8Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,
Yaani Misri.
Putu na Kanaani.
9Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
10Kushi akamzaa
Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.
11Misraimu akawazaa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
12Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
13Wana wa Kanaani walikuwa:
Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,
14Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15Wahivi, Waariki, Wasini, 16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu

17Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
18Arfaksadi akamzaa Shela,
Shela akamzaa Eberi.
19Eberi alipata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi,
Pelegi maana yake Mgawanyiko.
kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
20Wana wa Yoktani walikuwa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22Obali, Abimaeli, Sheba, 23Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

24Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,
25Eberi, Pelegi, Reu,
26Serugi, Nahori, Tera,
27Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).

Jamaa Ya Abrahamu

28Abrahamu alikuwa na wana wawili:
Isaki na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

(Mwanzo 25:12-16)

29Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:
Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura

32Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:
Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.
Wana wa Yokshani walikuwa:
Sheba na Dedani.
33Wana wa Midiani walikuwa:
Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.
Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara

34Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.
Wana wa Isaki walikuwa:
Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

(Mwanzo 36:1-19)

35Wana wa Esau walikuwa:
Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
36Wana wa Elifazi walikuwa:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;
Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.
37Wana wa Reueli walikuwa:
Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

(Mwanzo 36:20-30)

38Wana wa Seiri walikuwa:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39Wana wa Lotani walikuwa wawili:
Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani,
Maandishi ya Kiebrania yanamwita Alian.
Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana.
41Mwana wa Ana alikuwa:
Dishoni.
Nao wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

(Mwanzo 36:31-43)

43Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:
Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51Naye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi,
52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.
Copyright information for SwhNeno