‏ 2 Chronicles 33:21-25

Amoni Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 21:19-26)

21Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili, alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. 22Akatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya. Amoni akaabudu na kutoa dhabihu kwa sanamu zote alizokuwa ametengeneza Manase. 23Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za Bwana, badala yake Amoni aliongeza hatia zaidi na zaidi.

24Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani. 25Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.
Copyright information for SwhNeno